• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya jumla ya uchumi wa kidijitali wa China yafika dola trilioni 4.3 za kimarekani mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-04-13 16:40:09

    Mwaka jana thamani ya jumla ya uchumi wa kidijitali nchini China ilifikia dola trilioni 4.3 za kimarekani, na kuchukua asilimia 32.9 cha pato la taifa.

    Hayo yamo kwenye ripoti kuhusu maendeleo ya uchumi wa kidijitali wa China na utoaji wa nafasi ya ajira iliyotolewa na Taasisi ya teknolojia ya habari na mawasiliano ya China. Ripoti hiyo imesema, mwaka jana, idadi ya watu walioajiriwa kwenye sketa ya uchumi wa kidijitali ilifikia milioni 171, ambayo ilichukua asilimia 22.1 ya idadi ya jumla ya waajiriwa.

    Ripoti hiyo imeongeza kuwa, miaka ya hivi karibuni, uchumi wa kidijitali umekuwa injini kuu ya kuhimiza ongezeko la uchumi, ambapo mwaka jana mchango uliotolewa na uchumi wa kidijitali kwa pato la taifa ulifikia asilimia 55, na kufikia kiwango cha baadhi ya nchi zilizoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako