• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Urari mzuri wa biashara ya China na nje wapungua kwa asilimia 21.8

    (GMT+08:00) 2018-04-13 17:25:28

    Urari mzuri wa biashara ya China na nchi za nje ulipungua kwa asilimia 21.8 katika robo ya kwanza ya mwaka huu na kuifanya China ishuhudie uwiano mzuri zaidi wa biashara.

    Kwa mujibu wa Mamlaka Kuu ya Forodha ya China, uuzaji bidhaa za China nje ya nchi uliongezeka kwa asilimia 7.4 katika miezi mitatu ya kwanza ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho, huku uagizaji bidhaa kutoka nje ukiongezeka kwa asilimia 11.7 na kupelekea urari mzuri kufikia dola za kimarekani bilioni 51.85.

    Akizungumza na waandishi wa habari, msemaji wa Mamlaka hiyo Huang Songping amesema ongezeko la kuridhisha la biashara linatokana na ufufukaji taratibu wa uchumi wa dunia, ambao umechochea shughuli za kibiashara pamoja na maendeleo mazuri ya uchumi wa China, ambayo yameimarisha mahitaji kwa uagizaji bidhaa kutoka nje.

    Anasema, "Biashara ya China na nje inazidi kuwa na uwiano, na kasi ya ongezeko la uagizaji bidhaa kutoka nje ni asilimia 4.3 zaidi kuliko ile ya uuzaji bidhaa nje ya nchi, na urari mzuri wa biashara ya China na nje ulipungua kwa asilimia 21.8. Hii inaonesha kuwa China imefungua mlango zaidi kwa nchi za nje na kuzifanya zinufaike zaidi."

    Bw. Huang ameongeza kuwa maendeleo tulivu kwenye Mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja na biashara yenye nguvu kati ya China na masoko yaliyoibuka hivi karibuni pia vimechangia ongezeko katika robo ya kwanza. Amesema ukubwa wa biashara kati ya China na nchi za Ukanda Mmoja na Njia Moja uliongezeka kwa asilimia 12.9 katika miezi mitatu ya kwanza, ikiwa ni asilimia 3.5 zaidi kuliko kasi ya ongezeko la biashara ya jumla ya China na nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako