• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CPC yaunga mkono kisiwa cha Hainan kujenga eneo la majaribio la biashara huria

  (GMT+08:00) 2018-04-13 19:44:18

  Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kinaunga mkono kisiwa cha Hainan kujenga eneo la majaribio la biashara huria, kisiwa hicho kujaribu na kuhimiza ujenzi wa bandari ya biashara huria yenye umaalumu wa kichina, na kuanzisha sera na mfumo wa bandari ya biashara huria.

  Hayo yamesemwa na rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 30 ya kuanzishwa kwa mkoa wa Hainan na eneo maalumu la uchumi. Ametoa mwito kwa Hainan kufanya juhudi kujijenga kuwa mfano mpya wa China na kuimarisha zaidi mageuzi na ufunguaji mlango katika zama mpya, kutoa kipaumbele kwenye mageuzi ya sekta ya utoaji bidhaa, na kujenga eneo la majaribio ya biashara huria na bandari ya biashara huria yenye umaalumu wa kichina. Pia kutumia nguvu kujenga eneo la majaribio la mageuzi na ufunguaji mlango wa China, eneo la majaribio ya ikolojia la taifa, kituo cha matumizi ya kitalii cha kimataifa na eneo la kutoa huduma na kuhakikisha mkakati mkubwa wa taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako