• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Poland kuweka Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-04-13 20:08:06

  Ubalozi wa Poland nchini Tanzania umeahidi kuwekeza katika kutengeneza na kuunganisha matrekta katika Mkoa wa Pwani.

  Pia umeahidi kuwekeza katika utengenezwaji wa vifaa vya kisasa vya kuhifadhi nafaka kwa baadhi ya mikoa ili kuhakikisha ubora na viwango vya nafaka unaimarika ili kuepuka kupotea kwa mazao mengi.

  Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga alisema ni uamuzi sahihi kwa Poland kuanzisha upya ubalozi wake na utaongeza uhusiano mzuri na nchi zote. Alisema vipo vipaumbele mbalimbali vilivyowekwa na Poland na katika eneo la uhifadhi wa nafaka alisema uhifadhi bora wa nafaka ni moja ya fursa muhimu katika mnyororo mzima wa usambazaji wa chakula pamoja na kuchangia ubora katika lishe.

  Waziri Mahiga ameongeza kuwa hatua nyingine ambazo serikali ya Kipolishi itasaidia ni pamoja na maji, umwagiliaji na elimu ambayo wataanza kutoa elimu kwa Watanzania. Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Jacek Czaputowicz alisema ufunguzi mpya wa ubalozi wao ni hatua muhimu katika maendeleo ya uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili. Alisema Poland na Tanzania zina historia ya uhusiano wa kirafiki wa kisiasa, kufunguliwa kwa ubalozi wa Kipolishi kuna fursa ya kuwatia nguvu kwa kupata ujuzi na jukumu la Tanzania kulinda amani na usalama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako