• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya dunia yaonya kuwa milioni 16 huenda wakaendelea kuathiriwa na umaskini Kenya

  (GMT+08:00) 2018-04-13 20:08:25

  Benki ya dunia imeonya kuwa jumla ya watu milioni 16 huenda wakaendelea kuathiriwa na umaskini katika kipindi cha miaka 12 ijayo. Tangazo hili la Benki ya dunia linatokana na hofu ya kutokuwa na imani na juhudi za serikali za kuahidi kutoa mazingira ya maisha mazuri kwa wakenya wote ifikapo mwaka wa 2030.Benki ya dunia aidha imesema juhudi z aserikali zinafaa kwenda na vitendo na kuwashirikisha wakenya wote ili kwa pamoja taifa lifikie maendeleo yatakayomridhisha kila mkenya.Wakati idadi ya watu ikikadiriwa kufikia milioni 65.4 inakisiwa kuwa takriban watu milioni 16.4 kati yao wanatarajiwa kusalia kuwa maskini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako