• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yashambulia Syria

  (GMT+08:00) 2018-04-14 17:34:47

  Marekani imeanza mashambulizi dhidi ya Syria katika mji mkuu wa Damascus kabla siku ya jumamosi ambapo milio mikali yenye miale miekundu ya mabomu ilionekana katika anga.

  Milio ya sauti za milipuko ilisikika katika mji mkuu huo katika maeneo yote, huku majeshi ya anga yaSyria nayo yakionekana kurusha makombora yake kutokea mlima Qasion, ambao unatazamamana na mji mkuu wa Damascus.

  Mwenyekiti wa umoja wa wanadhimu wakuu wa majeshi ya marekani Joseph Dunford jana ijuma alisema mashambulizi hayo yanalenga maeneo kadha ya nchini Syria ikiwemo kituo cha utafiti , ghala la silaha za kikemikali na vituo vingine vya kuhifadhia silaha.

  Katika hatua nyingine, kituo cha televisheni cha Syria kimetangaza kuwa majeshi ya anga ya Syria yanajibu mashambulizi ya majeshi ya pamoja ya Marekani, Ufarasna na Uingereza.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi Hua Chunying amesema, China siku zote inapinga kitendo cha kimabavu katika mambo ya kimataifa, na kuzihimiza pande zinazohusika zirejee kwenye mazungumzo.

  Viongozi wa jumuiya ya kimataifa, pamoja na wakuu wa nchi tofauti tofauti akiwemo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutteres, Kiongozi wa Mkuu wa Kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na Rais wa Russia Vladmir Putin wamelaani kitendo cha Marekani na washirika wake cha kuishambulia Syria.

  Katika maneno yake aliyotoa ijumaa usiku, Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bw. Guterres ameeleza masikitiko yake juu ya uamuzi huo uliofanywa na Marekani, Ufaransa na Uingereza akisema kuna utaratibu wa kushughulikia masuala, hususani ya kulinda amani na usalama kimataifa kwa mujibu wa kanuni za umoja wa mataifa.

  Aidha, Katibu huyo amesema kanuni hizo zinazeleza kuwa, jukumu la kulinda amani na usalama wa kimataifa ni wajibu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, hivyo amewataka wajumbe wote wa baraza hilo kuungana na kutimiza wajibu wao

  Kwa upande wake, Rais Vladmir Putin wa Russia, yeye katika taarifa yake amesema mashambulizi yaliyofanywa na Marekani pamoja na washirika wake ni kitendo cha uchokozi dhidi ya taifa dhidi ya taifa huru na kwamba Russia inalaani kitendo hicho.

  Naye kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amezishutumu Marekani, Uingereza na Ufaransa kuyaita mashambulizi hayo ya anga dhidi ya Syria kuwa ni uhalifu.

  Kwa kusisitiza, Kiongozi huyo amewaita marais wa Marekani na Ufaransa pamoja na waziri mkuu wa Uingereza kuwa ni wahalifu waliotenda uhalifu dhidi ya Syria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako