• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonesho ya kimataifa ya Beijing ya filamu yafunguliwa

  (GMT+08:00) 2018-04-15 21:07:56

  Maonyesho ya 8 ya filamu ya kimataifa ya Beijing yamefunguliwa rasmi leo jioni.

  Maonyesho hayo yatafanyika kuanzia leo tarehe 15 hadi 22 ya mwezi huu. Katika miaka minane iliyopita, mashirika zaidi ya 1,600 ya filamu kutoka nchi mbalimbali duniani yameshiriki.

  Naibu katibu mkuu wa kamati ya maandalizi ya sikukuu ya kimataifa ya Beijing ya filamu Bw. Hu Dong amesema, mwaka huu filamu nyingi na bora zaidi zimeshiriki kwenye sikukuu hiyo, na inakadiriwa kuwa idadi na thamani ya makubaliano ya ushirikiano yatakayofikiwa vitazidi mwaka jana.

  Soko la filamu nchini China linakua kwa kasi sana, na thamani ya mauzo ya tikiti za filamu mwaka jana nchini humo ilifikia renminbi yuan bilioni 56, sawa na dola za kimarekani karibu bilioni 8.9.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako