• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri Mkuu wa Ethiopia asema serikali yadhamiria kujenga umoja ili kuleta maisha bora

  (GMT+08:00) 2018-04-16 08:30:18

  Waziri mkuu mpya wa Ethiopia Abiy Ahmed jana aliwahakikishia Waethiopia dhamira ya serikali yake ya kujenga umoja ili kuleta maisha bora.

  Bw. Ahmed ameyasema hayo wakati akihutubia Waethiopia wapatao elfu 25 pamoja na wanadiplomasia. Amewataka washiriki, wakiwemo maofisa kutoka serikali kuu na za majimbo, viongozi wa dini, wawakilishi wa wanawake na vijana, wasomi na wataalamu kutoka nyanja mbalimbali, kushirikiana pamoja kujenga amani na demokrasia, ili kuhakikisha utawala bora na uwajibikaji wa maofisa wa umma.

  Wito huo wa kuleta umoja ameanza kuutoa mapema wiki iliyopita ikiwa sehemu ya ziara yake rasmi ya kwanza nje ya mji mkuu Addis Ababa, katika jimbo la mashariki mwa Somalia, ikiwa na lengo la kutatua mapambano makali ya kijamii ambayo yamesababisha vifo vya mamia ya Waethiopia na maelfu kupoteza makazi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako