• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Bei ya sukari imeshuka kutokana na ushindani kati ya bidhaa za ndani na za nje.

  (GMT+08:00) 2018-04-16 19:32:55

  Bei za watumiaji wa sukari zimeshuka zaidi kutokana na ushindani kati ya bidhaa za ndani na za nje.

  Katika maduka mengi ya rejareja ya Nairobi, pakiti ya kilo mbili imeshuka kutoka juu ya Sh230 mwezi Januari na Februari hadi, Sh205 kwa sukari ya Kabras.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Sukari, kushuka imechangiwa na kushuka kwa bidhaa katika viwanda.

  Bei imeshuka katika viwanda kwa sababu ya ushindani kati ya sukari iliyoagizwa na ile iliyozalishwa ndani ya nchi.

  Tani ya sukari iliyoagizwa kwa wastani inauuzwa kwa Sh3,000 kwa tani wakati ile ya ndani inauuzwa kwa Sh3,600.

  Uagizaji wa sukari kutoka nje imenyima watengenezaji sukari wa ndani biashara.

  Mwaka jana bei ya sukari ilipanda hadi Sh400, na kulazimisha serikali kuingilia kati kwa kuondoa ushuru wa uagizaji bidhaa kutoka nje ya Soko la Pamoja la Afrika Mashariki na Kusini (Comesa), ambayo iliona wafanyabiashara kuingiza zaidi ya tani 900,000.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako