• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China akutana na mwenyekiti wa WEF

  (GMT+08:00) 2018-04-16 20:23:02

  Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na mwenyekiti wa Baraza la Uchumi Duniani WEF Bw. Klaus Schwab.

  Rais Xi Jinping amesema, historia imethibitisha kuwa, kufunga mlango hakuna njia, bali ni kufungua mlango na ushirikiano tu ndio kunafanya njia inakuwa pana zaidi. China ikiwa ni nchi inayowajibika, itashirikiana na jumuiya ya kimataifa kwa kufungua mlango, kutafuta kunufaishana ili kufanya umuhimu wake na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa kuleta matumaini, utulivu na mustakabali mzuri wa dunia. Ameongeza kuwa, ushirikiano kati ya China na WEF unaendana na mchakato wa kufungua mlango wa China. Pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha ushirikiano, kutafuta nguvu mpya kwa ajili ya ongezeko la uchumi la dunia, na kupata utatuzi halisi wa kutatua changamoto za dunia.

  Bw. Schwab amesema, WEF inapenda kuunga mkono kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kuhimiza ushirikiano wa muda mrefu na China katika maendeleo yenye uvumbuzi, na kufanya juhudi za pamoja katika kuimarisha mfumo wa usimamizi wa dunia na kuhimiza utatuzi wa masuala ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako