• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania kuajiri walimu 6,000 wa sayansi

  (GMT+08:00) 2018-04-17 09:46:38

  Serikali ya Tanzania inapanga kuwaajiri walimu 6,000 hadi kufikia Juni mwaka huu, ili kupunguza ukosefu wa walimu wa sayansi na hisabati nchini humo.

  Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Joseph Kakunda amesema kuwa, mpango huo unalenga kukomesha ukosefu wa walimu katika shule zote za serikali kabla ya mwaka 2020.

  Bw. Kakunda amezindua mpango huo katika mkutano wa bunge unaoendelea mjini Dodoma.

  Amesema serikali ya Tanzania inadhamiria kuinua ubora wa elimu na kuboresha miundombinu katika shule zote za serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako