• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Syria yasema iko tayari kushirikiana na OPCW kwenye uchunguzi

    (GMT+08:00) 2018-04-17 10:06:11

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa Syria Bw. Faisal Mekdad amesema serikali ya Syria iko tayari kushirikiana na Shirika la kupiga marufuku Silaha za Kemikali OPCW kwenye uchunguzi wake kuhusu shambulizi la kikemikali nchini humo.

    Shirika la habari la Syria SANA limemnukuu Bw. Mekdad likisema baada ya kupewa mwaliko na serikali ya Syria, tume ya uchunguzi ya OPCW imewasili mjini Damascus siku tatu zilizopita, na kukutana mara nyingi na serikali ya Syria kujadili kuhusu kushirikiana katika kufanya uchunguzi wa haki, uwazi na sahihi.

    Hadi sasa bado haijaelezwa jinsi uchunguzi wa OPCW unavyoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako