• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA yaanza kugakua nchi zilizoomba kuandaa kombe la dunia mwaka 2026, wataalam watua Morocco jana

    (GMT+08:00) 2018-04-17 10:25:27

    Timu ya wataalam kutoka FIFA imeanza kutembelea na kukagua nchi zilizoomba kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2026, ambapo jana imewasili nchini Morocco na inatarajia kuanza kazi leo April 17 hadi April 19.

    Baada ya zoezi la kukusanya taarifa kukamilika timu hiyo itaziwasilisha FIFA kwa ajili ya uamuzi ambao matokeo yake yatatolewa Juni 13 mjini Moscow.

    Nchi nyingine zilizoomba nafasi ya kuandaa michuano hiyo ni Mexico, Canada na Marekani, na hii ikiwa ni mara ya nne Morocco kuomba ikiwa tayari imeomba mara nne bila mafanikio, mwaka 1994, 1998 na 2010.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako