• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda kutoa chanjo ya kipindupindu katika kambi za wakimbizi kutoka Kongo

    (GMT+08:00) 2018-04-17 19:18:31

    Wizara ya afya nchini Uganda itaanza kutoa chanjo ya ugonjwa wa kipindupindu ili kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo katika kambi za wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC uliosababisha vifo vya watu 44 na wengine zaidi ya elfu 2 kulazwa tangu mwezi Februari.

    Kaimu mkurugenzi wa huduma za afya nchini humo Charles Olaro amesema, chanjo hiyo imepangwa kuanza mwezi ujao na itatolewa katika kambi za wakimbizi za Kyangwali na Kyaka II, ambazo ziko kwenye wilaya za magharibi za Hoima na Kyegegwa.

    Bw. Olaro amesema chanjo hiyo pia itatolewa katika maeneo mengine nchini Uganda ikiwemo Buliisa, Pakwach, Kasese, na Zombo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako