• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria wazuia makombora mengi yaliyolenga viwanja viwili vya jeshi la anga

  (GMT+08:00) 2018-04-17 19:19:15

  Vyombo vya habari vya Syria vimeripoti kuwa, mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria umefanikiwa kuzuia makombora mengi yaliyolenga viwanja viwili vya jeshi la anga nchini Syria leo alfajiri.

  Makombora sita yalirushwa kwa kulenga kiwanja cha ndege cha jeshi kilichoko Shayrat karibu na mkoa wa Homs katikati ya Syria, lakini mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria ulizuia baadhi ya makombora hayo. Makombora mengine matatu dhidi ya kiwanja cha ndege cha jeshi cha Dumair karibu na Damascus nayo yalizuiliwa na mfumo huo. Lakini bado haijathibitihwa makombora hayo yalirushwa kutokea wapi.

  Hata hivyo, Kituo cha televisheni cha Syria kimesema, taarifa za mashambulizi ya makombora dhidi ya viwanja viwili vya ndege vya kijeshi katika eneo la katikati na kusini mwa nchi hiyo si za kweli.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako