• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM apongeza uteuzi wa waziri mkuu wa Guinea-Bissau

    (GMT+08:00) 2018-04-18 09:34:17

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amepongeza kuteuliwa kwa Bw. Aristides Gomes kuwa waziri mkuu wa Guinea-Bissau na tangazo kuhusu uchaguzi wa bunge kufanyika Novemba 18 mwaka huu.

    Msemaji wa katibu mkuu wa UM Bw. Stephane Dujarric ametoa taarifa ikisema, Bw. Guterres amefurahishwa na moyo wa maelewano na uongozi uliooneshwa na rais Jose Mario Vaz na vyama vikuu vya kisiasa.

    Aidha amezitaka pande zote kuchukua hatua muhimu, zikiwemo kuunda serikali ya umoja, kufungua tena bunge la taifa na kutekeleza vipengele vilivyosalia vya makubaliano ya Conakry.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako