• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya Afrika yatajwa kuwania tuzo za kimataifa za Ashden

    (GMT+08:00) 2018-04-18 09:40:05

    Makampuni kadhaa madogo na ya ukubwa wa kati yanayotoa ufumbuzi wa kutochafua mazingira kwa sekta za nishati, ujenzi, afya, usafiri na fedha za Afrika, yametajwa kuwania tuzo kubwa duniani.

    Makampuni hayo yatashindana na makampuni mengine kutoka sehemu nyingine duniani kwenye tuzo za Kimataifa za Ashden zitakazowatunuku watangulizi wa kufanya uvumbuzi usiochafua mazingira. Mwanzilishi na mkurugenzi wa tuzo ya Ashden, Sarah Butler Sloss, amepongeza uvumbuzi wa kisasa ambao umeziwezesha jamii za nchi za dunia ya tatu kukabiliana na matokeo mabaya ya mabadiliko ya hali ya hewa.

    Miongoni mwa makampuni yanayotarajiwa kuzoa tuzo hiyo ni pamoja na kampuni ya Angaza ya Nairobi inayotoa huduma ya umeme wa jua kwa watu wasiounganishwa kwenye gridi ya taifa. Makampuni yaliyoteuliwa mwaka huu kupokea tuzo hiyo yamechaguliwa kutokana na mchango wao wa kutoa kaboni chache na mageuzi ya maisha ya watu wa sehemu zenye vikwazo vya rasilimali kama nchi za Afrika zilizo kusini mwa Sahara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako