• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu tatu za Afrika Mashariki zitakuwa ugenini kwa ajili ya mechi za marudiano

    (GMT+08:00) 2018-04-18 10:37:15

    Timu tatu za kutoka Afrika Mashariki, Gor Mahia ya Kenya, Young Africans ya Tanzania na Rayon Sport ya Rwanda zinashuka dimbani leo kwa ajili ya mechi za marudiano za hatua ya mtoano katika kombe la shirikisho barani Afrika.

    Gor Mahia itakuwa mjini Pretoria nchini Afrika Kusini kucheza na wenyeji wao Supersport United, na ili kusonga mbele mabingwa hao wa Kenya itawalazimu kulinda ushindi wa goli 1-0 waliopata katika mechi ya kwanza.

    Mabingwa wa Rwanda Rayon Sport, wao watakuwa nchini Msumbiji kurudiana na Costa Do Sol ambayo katika mechi ya awali wakiwa mjini Kigali waliifunga timu hiyo magoli 3-0.

    Nayo Young Africans inarudiana na Welayta Dicha ya Ethiopia mjini Sodo, lakini ikiwa na faida ya magoli 2-0 iliyopata kwenye mechi ya awali.

    Endapo timu hizo zitapa ushindi wa jumla baada ya mechi hizo, moja kwa moja zitafuzu na kujumishwa katika mechi za hatua ya makundi.

    Droo ya kupanga mechi za hatua ya makundi itafanyika jumamosi ijayo Aprili 21 mjini Cairo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako