• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka za Usalama nchini Australia zaahidi kumtafuta na kumpata Bondia Brian Agina wa timu ya Kenya 

    (GMT+08:00) 2018-04-18 10:38:49

    Polisi nchini Australia wamesema jitihada zinafanyika ili kumpata bondia chipukizi wa kiume ambaye alitoweka katika kambi ya timu ya Kenya iliyokuwa inashiriki michezo ya jumuiya ya madola mjini Gold Coast.

    Brian Agina mwenye miaka 19, bado hajaonekana tangu atoweke kambini jumapili iliyopita huku juhudi za kumpata zikifanyika kwa pamoja kati ya Mamlaka za usalama nchini Australia na ubalozi wa Kenya nchini humo.

    Kwa mujibu wa Ofisi ya uhamiaji ya Australia Brian bado ana kibali halali cha kuendelea kukaa nchini Australia kwa kuwa viza yake inaisha tarehe 15 ya mwezi mei licha ya kuwa michezo ya jumuiya ya madola imefungwa.

    Katika ushiriki wake kwenye mashindano hayo, Agina alishindwa kufuzu raundi ya pili baada ya kupigwa na Syed Muhammad wa Pakistan katika mechi ya kwanza.

    Kundi la mwisho la timu ya Kenya iliyokwenda Australia, linaondoka leo akiwemo kocha mkuu wa Agina amabye anashikilia pasi ya kusafiria ya bondia huyo.

    Agina sasa anakuwa mwanamichezo wa kumi kutoka Afrika aliyetoweka baada ya wengine nane kutoka Cameroun kutoonekana tangu wiki iliyopita na mmoja wa Tanzania aliyetangazwa kupotea kambini jumatatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako