Mchumi mkuu wa IMF Maurice Obstfeld, amezishauri nchi zinazotegemea mafuta kwa uchumi wao, kutafuta njia badala za kujiletea mapato ili kujikinga na athari za kushuka kwa bei ya mafuta.
Maurice anasema Uchumi wa Nigeria unatarajiwa kukua kwa asilimia 2.1 mwaka 2018 na asilimia 1.9 mwaka 2019 ukichangiwa na kuongezekwa kwa bei ya mafuta ambayo Nigeria inazalisha kwa wingi.
Kwa sasa pipa moja la mafuta kwenye soko la kimataifa linauzwa kwa dola 71.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |