• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TradeMark East Africa dola milioni 1.05 kuendeleza miundo mbinu Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2018-04-18 20:34:45

    Shirika la TradeMark East Africa (TMEA) na mamlaka ya kuratibu ushoroba wa kaskazini wa uchukuzi zimesaini makubaliano ya kutolewa kwa dola milioni 1.05 za kuendeleza miundo mbinu ya kanda ya Afrika Mashariki.

    TMEA itatoa fedha hizo kwa mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka 3 ijayo.

    Ufadhili huo utawezesha mamlaka hiyo kutathmini data inayohusiana na uchukuzi wa watu na bidhaa kwenye ushoroba wa kazkazini.

    Ushoroba huo ndio muhimu zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki ukianzia katika bandari ya Mombasa na baadaye kusambaa kupitia nchi za Rwanda, Uganda, Sudan Kusini Burundi na DR Congo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako