• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa UN aitaka Afrika kukumbatia kilimo cha uhifadhi kukabiliana na mabadiliko ya hali hewa

    (GMT+08:00) 2018-04-19 08:57:23

    Mtaalamu wa mazingira wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kutumia kilimo cha uhifadhi katika Afrika ili kuweza kuliokoa bara na mabadiliko ya hewa.

    Akiongea kwenye mkutano mjini Nairobi, Mratibu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mabadiliko ya hali ya hewa ya Afrika, Richard Munang, amesema kama watu hawakuwa waangalifu, mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kushusha uchumi wa Afrika kwa asilimia 75 katika miaka michache ijayo. Hivyo ametoa wito wa kutumia kilimo cha kisasa, akiongeza kuwa sekta za kilimo za nchi za Afrika zinaweza kuwa na matatizo mengine mengi yatakayotishia usalama wa chakula barani humo.

    Kulingana na mtaalamu huyo wa mazingira, tafiti zinaonesha kuwa kilimo cha uhifadhi kinaweza kuongeza mavuno hadi kufikia asilimia 128 chini ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha usalama wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako