• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wataka dunia kuijengea Somalia uwezo wa kukabiliana na vitisho vya ugaidi

    (GMT+08:00) 2018-04-19 09:30:03

    Tume ya Umoja wa Afrika ya Kulinda Amani nchini Somalia AMISOM imeitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia Somalia kuijengea uwezo wa kukabiliana na vitisho nchini humo.

    Wakihitimisha mkutano wa nne wa mwaka, Maafisa wakuu wa AMISOM wakiwemo maafisa wa usalama wamefikia makubaliano juu ya hatua za kukabiliana kwa ufanisi na tishio la mabomu ya kienyeji linalozuia mchakato wa kupata utulivu nchini humo.

    Mwakilishi maalum wa mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Francisco Madeira, amewapongeza washirika mbalimbali kwa kuendelea kuwaunga mkono na kujitolea askari wake kwa AMISOM kukabiliana na tishio la mabomu ya kienyeji (IED) kwa vikosi vya usalama na raia wa Somalia.

    Mapema mwezi huu Kitengo cha Huduma za kutegua Mabomu cha Umoja wa Mataifa kimesema takriban watu 3,000 wameuawa ama kujeruhiwa kutokana na mabomu hayo nchini Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako