• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mvua kubwa zasababisha wakenya kusumbuliwa na tatizo la maji

    (GMT+08:00) 2018-04-20 08:44:58

    Wakazi wa miji mbalimbali ya Kenya wanaosumbuliwa na tatizo la maji kwa muda mrefu, wameonyesha kufurahishwa na ujio wa mvua, wakidhani kuwa mvua hizo zitakuwa suluhisho kwa tatizo hilo.

    Hata hivyo mvua hizo ambazo zimekuwa zikiendelea kunyesha kwa muda wa mwezi mmoja sasa zimesababisha mafuriko, kukwamisha usafiri na kufanya baadhi ya watu kupoteza makazi.

    Katika eneo la Nairobi baadhi ya watu wameanza kupata maji kwa mgao kutokana na miundombinu ya maji kuharibiwa.

    Katika eneo la mto Tana familia elfu nane zimejikuta bila makazi baada ya maji ya mto Tana kuvunja kingo za mto na kuharibu nyumba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako