• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wahimiza uungaji mkono wa kimataifa kwa ufumbuzi wa kisiasa wa suala la Libya

    (GMT+08:00) 2018-04-20 08:47:06

    Kamati ya ngazi ya juu ya Umoja wa Afrika inayoshughulikia suala la Libya imeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama nchini Libya, na kulaani uingizaji wa silaha nchini humo. Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika baada ya mkutano wa tano wa kamati hiyo kufungwa Addis Ababa, inasema kamati hiyo inahimiza wadau wote wa kikanda na kimataifa kusitisha usafirishaji wa silaha nchini humo kwa mujibu wa maazimio husika ya Baraza la usalama la Umoja wa mataifa. Kamati hiyo pia imesisitiza kuunga mkono umoja wa Libya na kulaani kitendo chochote kinacholeta mgawanyiko wa kikabila nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako