• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lagarde atoa mwito wa kuondoa hatua zote za kujilinda kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-04-20 10:01:57

    Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani IMF Bibi Christine Lagarde amewataka watunga sera wa nchi mbalimbali kuondoa hatua zote za kujilinda kibiashara na kuendelea kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi.

    Akikutana na wanahabari kando ya mkutano wa IMF na Benki ya Dunia uliofanyika huko Washington, Bibi Lagarde amesema hatua za upande mmoja za kuzuia biashara hazijathibithwa kuwa na ufanisi, na hata zinaweza kupunguza imani ya wawekezaji, na kwamba nchi mbalimbali zinapaswa kutatua kwa pamoja migogoro yao bila kutumia hatua zisizo za kawaida.

    Bibi Lagarde pia amesema IMF itaendelea kusisitiza manufaa ya utaratibu wa biashara wa pande nyingi ulio wazi na kujengwa kwenye msingi wa kanuni, na kuzitaka nchi mbalimbali kuchukua hatua zaidi ili kutokomeza vizuizi vya kibiashara na visivyo vya kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako