• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sekta ya safari ya anga ya juu ya China yapata maendeleo ya kasi

  (GMT+08:00) 2018-04-20 16:54:37

  Tarehe 24 ni siku ya tatu ya safari za anga ya juu ya China. Mwaka huu kauli mbiu ya siku hiyo ni kujenga zama mpya ya safari za anga ya juu kwa pamoja.

  Msemaji wa idara ya safari ya anga ya juu ya China Bw. Li Guoping jana kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, tangu tarehe 24 Aprili mwaka jana, China imerusha vyombo vya safari za anga ya juu mara 25, na kupeleka satilaiti 53 angani. Wakati huo huo China ilipata mafanikio mengi muhimu katika utafiti wa sayansi na teknolojia za anga ya juu na matumizi ya teknolojia hizo. Amedokeza kuwa, mwaka huu China itarusha satilaiti ya Chang'e No. 4 na chombo cha utafiti katika sayari ya mwezi. Anasema,

  "Mradi wa utafiti wa sayari ya mwezi wa Chang'e No. 4 na No. 5 unaendelea vizuri kama ulivyopangwa. Chombo cha Chang'e No. 4 kinatengenezwa na kitarushwa mwaka huu. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa binadamu kufikisha chombo cha utafiti nyuma ya sayari ya mwezi."

  Habari zinasema chombo cha Chang'e No. 4 pia kitabeba zana nne za utafiti za nchi za nje zikiwemo Ujerumani na Uholanzi.

  Bw. Li amesema sekta ya safari ya anga ya juu ya China imefungua ukurasa mpya. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, satilaiti za matumizi ya umma zimetoa picha zaidi ya milioni 10, na wateja wa televisheni zinazotumia satilaiti wamezidi milioni 70. Anasema,

  "Hivi sasa tuna satilati zaidi ya 200 angani. Teknolojia za anga ya juu zinaharakishwa kuungana na teknolojia nyingine za kisasa. Wastani wa ukuaji wa sekta ya satilaiti kwa mwaka unazidi asilimia 20. Teknolojia za anga ya juu ni njia muhimu ya kuhudumia maendeleo ya uchumi na jamii, na pia zinasaidia sana uwiano wa maendeleo ya sehemu mbalimbali, na utekelezaji wa mkakati wa kustawisha vijiji.

  Wakati huo huo, mashirika ya kibiashara yanayoshughulikia safari za anga ya juu pia yamepata maendeleo ya haraka. Bw. Li anasema,

  "Takwimu zetu zinaonesha kuwa hadi sasa idadi ya mashirika makubwa yanayoshughulikia ubunifu, utengenezaji na matumizi ya satilaiti, roketi na vyombo vingine vya safari ya anga ya juu nchini China imezidi 30. Mashirika hayo yamepigia hatua katika utafiti wa satilaiti na roketi ndogo."

  Bw. Li ameeleza kuwa China itahimiza ushirikiano kati ya mashirika binafsi na upande wa jeshi katika safari za anga ya juu kwa mujibu wa "mpango wa mwaka 2025 wa utengenezaji wa China", na kuifanya sekta ya safari za anga ya juu iwe moja ya sekta mpya za kimkakati zinazoendelea kwa kasi nchini China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako