• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ataka kujenga taifa lenye nguvu kwenye mtandao

    (GMT+08:00) 2018-04-21 19:30:13

    Rais Xi Jinping wa China ametoa mwito wa kushika vizuri fursa za kihistoria zinazotokana na maendeleo ya teknolojia ya habari na kujenga China iwe taifa lenye nguvu katika mtandao wa internet.

    Rais Xi ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa kitaifa kuhusu kazi za usalama wa mtandao wa internet na maendeleo ya teknolojia ya habari uliofanyika jana na leo hapa Beijing. Pia amesisitiza umuhimu wa kulinda usalama kwenye mtandao wa internet, kumiliki teknolojia kuu kwenye sekta ya mawasiliano ya habari, kufanya maendeleo ya teknolojia ya habari yahudumie ukuaji wa uchumi, na kujiunga na mchakato wa usimamizi wa mtandao wa internet dunian ili kutoa mchango mpya kwa ajili ya kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, kupata ushindi wa ujamaa wenye umaalumu wa kichina na kutimiza ustawishwaji wa taifa la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako