• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na India wakutana Beijing

    (GMT+08:00) 2018-04-23 10:10:37

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw Wang Yi jana alikutana na mwenzake wa India Bibi Sushma Swaraj mjini Beijing.

    Bw Wang Yi amesema kwamba rais Xi Jinping wa China atafanya mkutano usio rasmi na waziri mkuu wa India Bw Narendra Modi tarehe 27 na 28 mwezi huu mjini Wuhan mkoani Hubei, China. Nchi zote mbili zinatakiwa kufanya maandalizi ili kufanikisha mkutano huo, kuzidisha ushirikiano kati ya pande mbili, na kutoa mchango katika kuhimiza maendeleo na amani ya kikanda na ya dunia nzima.

    Kwa upande wake Bibi Sushma Swaraj amesema India inapenda kushirikiana na China kuhimiza urafiki na kuinua kiwango cha kuaminiana, na kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako