• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu waipongeza China kwa kupata maendeleo makubwa katika uchumi wa kidijitali

    (GMT+08:00) 2018-04-23 16:47:24

    Ikiwa imetimia miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, mkutano wa kwanza wa kilele wa kujenga China ya kidijitali umefanyika huko Fuzhou, kusini mashariki mwa China. Washiriki wa mkutano huo wanaona mkutano huo utaifahamisha zaidi dunia kuhusu maendeleo iliyopata China katika sekta ya uchumi wa kidijitali katika miaka ya hivi karibuni, kuhimiza mawasiliano na mabadilishano ya uzoefu kati ya China na nchi za nje na kuimarisha zaidi ushirikiano.

    Mkutano wa kwanza wa kilele wa kujenga China ya Kidijitali wenye kauli mbiu ya "kufanya maendeleo ya teknolojia ya habari kuhimiza mambo ya kisasa na kuongeza kasi ya kujenga China ya kidijitali" unakusanya nguvu za pande mbalimbali kuhimiza ujenzi wa China ya kidijitali. Katika mkutano huo, wageni wa ndani na nje ya China kutoka sekta ya biashara na taaluma wametoa mapendekezo kwa ajili ya kuhimiza ujenzi wa China ya kijiditali.

    Mwenyekiti wa kampuni ya Inspur ya China Bw. Sun Pishu anasema watu wa kawaida wananufaika zaidi na maendeleo ya uchumi wa kidijitali wa China.

    "Maendeleo ya uchumi wa kidijitali katika miaka ya hivi karibuni yameboresha na kurahisisha maisha ya watu. Shughuli zote maishani zinaweza kufanywa kupitia simu ya mkononi, na huwezi kuendesha gari bila ya mfumo wa uongozaji safari."

    Bw. Sun pia anaona kuwa katika siku za baadaye, China inapaswa kuinua kiwango cha maendeleo ya teknolojia ya habari, kuboresha huduma za serikali na kupoteza muda wa watu katika kushughulikia shughuli hizo. Pia ni lazima kuhimiza ujenzi wa mtandao wa kiviwanda, na kufanya uchumi wa kidijitali uhudumie zaidi uchumi halisi.

    Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Alibaba Bw. Ma Yun amesema hivi sasa China imeongoza duniani katika mambo mbalimbali kuhusu teknolojia ya dijitali, lakini katika ubunifu wa teknolojia muhimu, kampuni za China zinapaswa kubeba wajibu zaidi.

    "Naona kampuni kubwa halisi hazipaswi kuangalia kama zimepata soko kubwa kiasi gani, bali ni kuzingatia kama zinamiliki teknolojia kuu na muhimu. Kampuni kubwa zinabeba wajibu usioweza kukwepeka katika kupata teknolojia kuu zinazohusu maendeleo ya jamii na binadamu."

    Mtafiti wa Umoja wa Mataifa profesa Banji Oyelaran-Oyeyinka amesema China imepata maendeleo ya kasi katika ulipaji wa kutumia simu ya mkononi na manunuzi kwenye mtandao wa internet, na kutoa mifano mizuri kwa nchi nyingine.

    "Maendeleo iliyopata China ni ya kasi na kushangaza. China imetupatia moyo kuwa inawezekana kupata maendeleo ndani ya muda mfupi. Maarifa ya China imeonesha kuwa uchumi wa kidijitali unaweza kuungana kwa kina na uchumi halisi, kuboresha maisha ya watu, kuinua sifa ya maisha. Pia tumeona kuwa uchumi wa kidijitali unaweza kuhimiza maendeleo yenye usawa na kuyawezesha makundi ya watu yanayoweza kusahaulika kujiunga na jamii."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako