• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shinikizo la juu la damu husababisa upofu na kifo

    (GMT+08:00) 2018-04-23 18:18:07

    Shinikizo la juu la damu ni miongoni mwa maradhi yanayoendelea kuwapata watu wengi nchini na duniani kwa ujumla. Kila siku idadi ya watu wenye maradhi haya ambayo yapo kwenye kundi la yasiyo ya kuambukiza huongezeka. Ugonjwa huu jinsi ulivyo ni kuwa baada ya kuathiri mfumo wa damu husababisha madhara sehemu mbalimbali za mwili yakiwemo macho.

    Kwa vile huanzia kwenye mfumo wa damu madhara yake kwenye macho huhusisha mishipa ya damu iliyo ndani ya jicho hususan sehemu ya ndani ya ukuta wa nyuma inayoitwa retina. Kazi kubwa ya retina ni kupokea mwanga wenye taswira na kuubadilisha kwenye mfumo utakaowezesha taswira kusafirishwa mpaka kwenye ubongo kwa ajili ya kutafsiriwa.

    Shinikizo la juu la damu husababisha kuta za mishipa ya damu kutanuka ikiwemo iliyomo kwenye retina. Kadri kuta za mishipa ya damu inavyotanuka ili kukabiliana na ongezeko la msukumo wa damu kutoka kwenye moyo ndivyo inavyosababisha upenyo wa ndani ya mishipa hii ya damu kupungua.

    Kupungua kwa upenyo huu hupunguza kiwango cha damu kinachoweza kupita kwenye mishipa hii. Upunguaji huu wa damu husababisha kiasi kidogo cha damu kufika kwenye retina.

    Kukosekana huku kwa kiwango kinachostahili cha damu ambayo hubeba virutubisho na hewa safi na kuipeleka kwenye chembe hai hufanya uchukuaji wa uchafu kwa ajili ya kuusafirisha mpaka kwenye ogani ambazo hufanya kazi ya kuuondoa ushindikane. Damu hii inavyopungua hupelekea ukosefu wa virutubisho kwenye chembe hai zinazounda retina hivyo kusababisha retina kushindwa kufanya kazi yake sawasawa. Na matokeo yake kwa mgonjwa huwa ni kushindwa kuona vizuri.

    Sababu kubwa ya kutokea kwa athari za shinikizo la juu la damu kwenye macho ni kupanda kwa shinikizo la damu. Madhara haya kwenye retina hutokea baada ya mgonjwa kuwa na shinikizo la juu la damu kwa muda mrefu, kwa miaka kadhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako