• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuelekea mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga: Mechi haitabiliki

    (GMT+08:00) 2018-04-24 08:36:43
    Wakati watani wa jadi Simba na Yanga zinakutana mwishoni mwa wikiendi hii jijini Dar es Salaam katika mchezo wao wa pili wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2017/18, Simba ndiyo wanaongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi.

    Safu ya ushambulizi ya Simba inaonekana kuwa kali zaidi baada ya wachezaji wake kukwamisha wavuni mabao 58 katika mechi 25.

    Watani wao Yanga ambao wamecheza mechi 23 wanafuatia wakiwa na mabao 40 ya kufunga.

    Mechi ya watani hao, mara nyingi inakuwa haitabiriki na imekuwa ikitokea timu inayoonekana bora wakati mwingine kupoteza dhidi ya timu ambayo inaonekana si bora sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako