• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matetemeko ya ardhi yanaweza kutabiriwa kwa mujibu wa vitendo vya wanyama?

    (GMT+08:00) 2018-04-24 09:26:34

    Baadhi ya wakati watu walishuhudia vitendo vya ajabu vya wanyama kabla ya matetemeko ya ardhi, lakini ripoti mpya iliyotolewa kwenye gazeti la shirika la matetemeko ya ardhi la Marekani inasema vitendo vya wanyama haviwezi kutumiwa kutabiri matetemeko ya ardhi.

    Watafiti cha kituo cha jiolojia cha Ujerumani wamechambua ripoti 729 za vitendo vya ajabu vya wanyama kabla ya matetemeko 160 ya ardhi, ambazo zinahusu wanyama wa aina mbalimbali ikiwemo tembo na nondo wa hariri, na kugundua kuwa ripoti hizi kimsingi ni mambo yaliyotokea mara moja tu au habari ambazo haziwezi kutumiwa kama ushahidi.

    Watafiti wamesema ni vigumu kuthibitisha kama vitendo vya ajabu vya wanyama ni dalili ya matetemeko ya ardhi au la, kwa sababu watu hawajawahi kuchunguza vitendo vya wanyama kwa muda mrefu kabla ya matetemeko ya ardhi.

    Watafiti wamesema inaonekana kwamba huwa inaokea tu wanyama kufanya vitendo vya ajabu, au huenda wanaweza kuhisi mawimbi ya matetemeko, mabadiliko ya maji na hewa chini ya ardhi kabla ya matetemeko ya mwanzo kutokea. Lakini matetemeko ya mwanzo yanatokea mara chache tu kabla ya matetemeko ya ardhi

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako