• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mawaziri wa ulinzi wa SCO

    (GMT+08:00) 2018-04-24 10:12:08

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na mawaziri wa ulinzi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai SCO mjini Beijing.

    Rais Xi Jinping amesema Mkutano wa mawaziri wa ulinzi utakaofanyika kesho utakuwa ni wa kwanza kufanyika tangu nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuongezeka. Amesema anaamini kuwa kutokana na ushirikiano wa pande zote, mkutano huo utaingiza nguvu mpya na mambo mapya kwenye maendeleo ya Jumuiya ya ushirikiano wa Shanghai.

    Waziri wa ulinzi wa Russia Bw. Sergey Shoigu akiwawakilisha wenzake wa nchi wanachama wa SCO, amesema wana imani kuwa kwa kufuata maelekezo ya rais Xi Jinping na viongozi wa nchi mbalimbali, ushirikiano wa ulinzi wa jumuiya hiyo utatoa mchango muhimu katika kulinda maslahi ya kimkakati ya nchi mbalimbali, pamoja na amani na utulivu wa kikanda na dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako