• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Chantal Umutoni Kagame ateuliwa kama Afisa Mkuu wa Biashara MTN Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-04-24 20:29:03

    MTN Rwanda imemteua Chantal Umutoni Kagame kama Afisa Mkuu wa Biashara na pia afisa wa mawasiliano.

    Kabla ya uteuzi huo Kagame alikuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo Rwanda ambayo hivi karibuni ilinunuliwa na Bharti Airtel Ltd.

    Maafisa wa MTN Rwanda walithibitisha uteuzi wake kwenye nafasi hiyo ambayo ni mpya kwa kuwa idara ya mawasilaino awali ilikuwa chini ya iadara ya nguvu kazi.

    Kagame ambaye ni mtaalamu wa mawasiliano, ana uzoefu wa miaka 17 katika sekta hiyo.

    Alijiunga na Tigo Rwanda mwaka 2009 akiwa mkuu wa idara ya usambazaji wa mauzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako