• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Barabara tano Kampala kukarabatiwa

    (GMT+08:00) 2018-04-24 20:30:24

    Kwa jitihada za kuboresha usafiri katika maeneo ya miji, Mamlaka ya Jiji la Kampala (KCCA) inapanga kuboresha barabara kadhaa ambazo sasa ziko kwenye hali mbaya.

    Baadhi ya barabara hizo ni pamoja na Nakawa-Ntinda barabara ya John Babiha / Acacia Avenue, barabara ya Kabuusu-Bunamwaya-Lweza na ile ya Lukuli.

    Kwa mujibu wa tovuti ya KCCA, barabara tano zitakazokarabatiwa ziko katika kundi la pili la Mradi wa Maendeleo ya Taasisi ya Kampala (KIIDP-2).

    Mkurugenzi wa masuala ya umma na ushirika wa KCCA Peter Kaujju, amesema ukarabati wa barabara hizo uttanza mwezi ujao.

    Mradiwote wa ukarabati utachukua miaka mitano ukigharimu shilingi bilioni 77 na unafadhiliwa na Benki ya Dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako