• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utafiti waonesha kulala mchana kwa zaidi ya saa moja ndio chanzo cha kisukari

  (GMT+08:00) 2018-04-24 20:32:44

  Kusinzia mchana kwa zaidi ya saa moja ni dalili ya kisukari aina ya pili (type 2 diabetes), utafiti unasema. Utafiti huo wa kwanza wa aina yake uliofanywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Tokyo, Japan unabainisha uwekezano huo.

  Watalaamu hao walioongozwa na Dk Yamada Tomahide walipitia tafiti 21 zinazohusisha kiasi cha usingizi na uwezekano wa kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza; kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na kupooza ambazo zilihusisha watu 307,237 kutoka bara la Asia na nchi za magharibi.

  Watafiti hao waligundua kuwa kusinzia kwa muda unaozidi dakika 60 kunaongeza hatari ya kupata kisukari aina ya pili kwa asilimia 45 tofauti na kusinzia kusikozidi dakika 40.

  Uchambuzi wa taarifa walizokuwa nazo wataalamu hao, ulidhihirisha kwamba hakuna hatari yoyote kwa mtu anayesinzia mpaka dakika 40 lakini hatari huongezeka ghafla baada ya kuzidi dakika 60.

  Zipo sababu nyingi zinazoweza kuchangia hatari hiyo. Wanasema usingizi mrefu wa mchana unaweza kumaanisha kuwa mtu hakulala vizuri usiku suala linalohusishwa na msongo wa mawazo ambao ni chanzo cha kisukari.

  Akitoa maoni juu ya majibu ya utafiti huo, Profesa Naveed Sattar, daktari bingwa wa magonjwa ya metaboliki kutoka Chuo Kikuu cha Glasgow, Uingereza anasema: "Utafiti huu unaonyesha uhusiano wa kisukari na usingizi mrefu wa mchana. Inawezekana kinachosababisha kisukari ndio kinacholeta usingizi huo. Inawezekana ni sukari imezidi mwilini hivyo usingizi mrefu kuwa dalili ya kisukari."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako