• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito kuimarisha ushirikiano wa SCO katika ulinzi na usalama

    (GMT+08:00) 2018-04-25 10:09:19

    Mjumbe wa taifa na waziri wa ulinzi wa China Bw. Wei Fenghe ametoa wito kwa wenzake wa nchi wanachama za Shirika la Ushirikiano la Shanghai SCO kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo na kuendelea kuongeza ushirikiano wa ulinzi na usalama.

    Akihutubia mkutano wa 15 wa mawaziri wa ulinzi wa nchi za SCO uliofanyika mjini Beijing, Bw. Wei amesema nchi hizo zinatarajia kuendelea kushirikiana katika hali ya usawa, kusaidiana na kukabiliana na changamoto kwa pamoja, ili kujenga mfumo mzuri wa kulinda usalama wenye manufaa kwa wanachama wote.

    Habari zinasema Bw. Wei amekutana na wenzake wa Pakistan, Tajikistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan na India na kubadilishana nao maoni kuhusu kuongeza mawasiliano na ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako