• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa ripoti kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2018-04-25 10:26:37

    Siku tano baada ya Marekani kutoa ripoti ya haki za binadamu duniani kuelezea maoni yake kuhusu hali ya haki za binadamu katika nchi mbalimbali duniani kwa mwaka 2017, China imetoa ripoti ya haki za binadamu nchini Marekani kwa mwaka huo, ikionyesha mlolongo wa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Marekani.

    Ripoti hiyo iliyotolewa na ofisi ya baraza la serikali ya China inasema, kwa mara nyingine tena Marekani inajifanya ni "mlinzi wa haki za binadamu" na "jaji wa haki za binadamu" wakati rekodi yake yenyewe ya haki za binadamu ni chafu na inaendelea kudorora.

    Ripoti hiyo imetaja ukiukaji mkubwa wa haki za kiraia, ubaguzi wa rangi wa makusudi, dosari nyingi kwenye demokrasia ya kimarekani, kupanuka kwa pengo kati ya matajiri na masikini, ubaguzi na kutotendewa haki kwa makundi maalum kama wanawake, watoto na walemavu, na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako