• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuhimiza mtindo wa ushirikiano kati ya mitaji ya serikali na ya kijamii kwenye sekta ya utalii

    (GMT+08:00) 2018-04-25 18:27:07

    Wizara ya utamaduni na utalii na wizara ya fedha ya China zimetoa waraka wa pamoja ukipendekeza kuhimiza mtindo wa ushirikiano kati ya mitaji ya serikali na ya kijamii kwenye sekta ya utalii.

    Waraka huo umesema, China itaweka kipaumbele kwenye kuunga mkono mtindo wa ushirikiano kati ya mitaji ya serikali na ya kijamii katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vivutio vya utalii, wilaya za kitalii, na utalii vijijini.

    Wakati huohuo, waraka huo pia umezitaka idara za fedha za ngazi mbalimbali na idara za utalii kuhimiza fedha na mitaji ya jamii kuwekezwa katika sekta za utalii na kuhamasisha sekta ya watu binafsi kushiriki kwenye ujenzi wa miradi ya mtindo huo na kutoweka masharti yanayozuia au kuinua ovyo kiwango cha ushirikishwaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako