• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Mashariki yatesa AFCON

    (GMT+08:00) 2018-04-26 08:12:57
    Timu za Tanzania, Rwanda na Uganda zimefuzu raundi ya pili ya michuano ya kuwania kufuzu fainali za kombe la Mataifa Afrika (AFCON) kwa vijana chini ya umri wa miaka 20.

    Timu hizo za ukanda wa Afrika Mashariki zilifuzu hatua hiyo baada ya kushinda mechi zake za marudiano. Fainali za michuano hiyo zimepangwa kufanyika mapema mwakani nchini Niger.

    Tanzania, Ngorongoro Heroes imefuzu hatua hiyo kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 6-5 katika mechi iliyochezwa Kinshasa dhidi ya wenyeji wao Congo DR.

    Rwanda ilifuzu raundi ya pili kwa faida ya bao la ugenini ambapo ilitoka sare ya 1-1 mjini Nairobi dhidi ya wenyeji Kenya kabla ya kutoka suluhu mjini Kigali nayo Uganda imesonga mbele kwa jumla ya mabao 8-1 baada ya kushinda 5-1 nyumbani dhidi ya Sudani Kusini kabla ya kushinda 3-0 ugenini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako