• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rasilimali yenye ukubwa wa nanomita kadhaa inaweza kuzuia mpunga usivute sumu ya risasi

    (GMT+08:00) 2018-04-26 10:11:02

    Madini ya risasi kwenye udongo yakivutwa na mpunga, yatalimbikizwa kwenye mchele, na kuathiri vibaya sifa ya michele na usalama wa chakula. Hivi karibuni watafiti wa idara ya fizikia ya hali ya yabisi ya taasisi ya sayansi ya China wamegundua jinsi rasilimali ya Nano-Hydroxyapatite inavyozuia sumu ya risasi isiingie kwenye mchele.

    Rasilimali hiyo ina uwezo mkubwa wa kuvuta risasi, na hutumiwa katika kazi ya kuondoa uchafuzi wa maji na udongo. Lakini jinsi rasilimali hiyo inavyoweza kuzuia sumu ya risasi isiingie kwenye mchele bado haijulikani.

    Baada ya kufanya utafiti kwa kina, watafiti wamegundua kuwa baada ya rasilimali hiyo kuingia kwenye seli za mizizi ya mpunga, inaweza kuvuta risasi, kuifanya risasi kuanguka ndani ya seli hizi, kuzuia sumu hiyo isiathiri ukuaji wa mizizi na kuhamia sehemu ya juu ya mimea kutoka kwenye mizizi.

    Utafiti huo umethibitisha uwezo wa rasilimali yenye ukubwa wa nanomita kadhaa katika kuzuia mpunga usivute sumu ya risasi, na utatoa mchango mkubwa katika kuhakikisha usalama wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako