• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Kigali yaondoa vikwazo vya kuwekeza

    (GMT+08:00) 2018-04-26 19:08:00

    Halmashauri ya masuala ya jiji la Kigali imefanya marekebisho kadhaa katika yatakayotoa fursa zaidi za uwekezaji katika sekta ya ujenzi.

    Marekebisho hayo yatawezesha upatikanaji wa vibali vya kujenga ,vibali vya mazingira na geografia.

    Kwa sasa mda utaratibu wa kupata stakabadhi za ujenzi ni umepunguzwa hadi siku 7 kutoka 15 na kupata kibali haswa ni siku 50 kutoka 113.

    Benki ya dunia mwaka jana iliangazia ugumu wa upatikanaji vibali vya ujenzi jijini Kigali.

    Rwanda iliorodheshwa katika nafasi ya 112 miongoni mwa nchi 190 duniani.

    Meya wa jiji la Kigali Porfait Busabizwa amesema hatua hiyo itavutia wafanyibiashara na wawekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako