• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taasisi inayoangalia Uwazi na Uwajibikaji Tanzania yapongeza mradi wa ujenzi wa barabara za juu

    (GMT+08:00) 2018-04-27 18:53:46

    Mwenyekiti wa Taasisi inayoangalia Uwazi na Uwajibikaji katika Utekelezaji wa Miradi ya Miundombinu nchini Tanzania Bw. Kazungu Magile amesema mradi wa ujenzi wa barabara za juu (flyover) katika eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam, umezingatia thamani ya fedha huku mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi za Shirikia la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ukiwa na makandokando.

    Amesema ufuatiliaji wa taasisi hiyo kwa miradi mitatu, umebaini kuwa utekelezaji wa mradi wa flyover ya TAZARA katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Mandela, unaotekelezwa na Wakala wa Barabara nchini humo (TANROADS) kwa ufadhili wa JICA, umezingatia thamani ya fedha.

    Magile amesema hali hiyo ni tofauti kwa upande wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi wa Dungu, unaofanywa na NSFF na kugharimu Shilingi bilioni 87.3, na miradi ya maji.

    Alisema mradi wa makazi haukutekelezwa kulingana na malengo matano ya mradi, ambapo lengo la kwanza lilikuwa ni nyumba hizo ziletee shirika mapato, lakini hadi sasa hakuna hata nyumba moja iliyouzwa.

    Alisema pia mradi huo ulilenga kusaidia kuwainua wakandarasi wa ndani, lakini katika utekelezaji wa mradi huo asilimia 90 ya wakandarasi walikuwa wa nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako