• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi mawili ya mabomu nchini Afghanistan yafikia 23

  (GMT+08:00) 2018-04-30 18:53:31

  Watu 23 wameuawa wakiwemo washambuliaji wawili na wengine 27 kujeruhiwa katika mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotokea kwenye eneo lenye ofisi za balozi za nchi za nje katikati ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, leo asubuhi.

  Polisi mjini Kabul wamesema, mtu mmoja aliyekuwa akiendesha pikipiki alijilipua katika eneo la Shash Darak, wilaya ya 9 ya kipolisi mjini humo majira ya saa mbili asubuhi kwa saa za huko, huku mlipuko wa pili ukitokea dakika 40 baadaye baada ya timu za uokoaji, polisi na waandishi wa habari kufika kwenye eneo hilo.

  Hakuna kundi lililokiri kuhusika na mashambulizi hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako