• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utata kodi ya mafuta ghafi

    (GMT+08:00) 2018-04-30 19:53:54

    KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeiagiza serikali kuingilia kati utata wa kodi inayopaswa kulipa kwenye meli mbili za mafuta zilizotia nanga katika Bandari ya Dar es ili kuepusha upandaji bei wa mafuta ya kula na bidhaa zingine zitokanazo na mafuta ghafi.

    Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Suleiman Murad wakati wa semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo wabunge kuhusu utendaji kazi na majukumu ya taasisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Tume ya Ushindani (FCC) na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela).

    Murad anasema, mafuta ya kula yameanza kupanda bei, kwa sababu watu wa viwanda wameanza kutumia mafuta yaliyopo nchini hivyo kuishiwa na malighafi.

    Bunge lilipitisha kuwa kodi katika mafuta ghafi iwe ni asilimia 10 na kwa mafuta yaliyosafishwa kidogo kodi yake ni asilimia 25.

    Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya alisema suala hilo litashughulikiwa na ngazi za juu za maamuzi katika kufikia muafaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako