• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Deni kubwa ya umma ya sababisha bajeti kukatwa

    (GMT+08:00) 2018-04-30 19:55:39

    Bunge la Taifa limependekeza kupunguzwa kwa asilimia 6.6 katika matumizi ya bajeti ya maendeleo katika bajeti ya pili ya ziada ya 2017/2018 ili kufikia gharama kubwa ya madeni ya umma

    Kamati ya bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung'wah anataka Sh bilioni 40.8 bilioni kukatwa katika bajeti ya maendeleo ili kushughulikia mikopo ya ndani na ya nje, ambayo imeongezeka sana, na kufikia Sh bilioni 24.34.

    Kamati imeonyesha wasiwasi na kupunguzwa kwa bajeti ya maendeleo kwa kiasi kikubwa.

    Mnamo Februari, mapato halisi ya kitaifa yalikusanywa yaliongezeka na kufikia Sh bilioni 1.015 ambayo ilifikia asilimia 44 ya bajeti ya jumla ya mwaka.

    Kenya inakabiliana na madeni makubwa ya umma ambayo yanatishia kufika Sh trilioni 5. Kulingana na uchunguzi wa kiuchumi 2018, madeni ya nchi ni Sh trilioni 4.54 .

    Jumla ya deni imefikia asilimia 51.9 ya mikopo ya kigeni na asilimia 48.1 ya mikopo ya ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako