• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zambia azindua mpango wa kupanda miti

    (GMT+08:00) 2018-05-01 10:07:52

    Rais Edgar Lungu wa Zambia amezindua mpango wa kuhamasisha watu kupanda miti na kuhimiza maendeleo ya uchumi kwa kutegemea miti, ikiwa ni sehemu ya ajenda ya nchi hiyo kufanya uchumi wake kuwa na vyanzo mbalimbali.

    Viongozi wa Zambia wanakubaliana kuwa Zambia ni moja ya nchi zilizoko kusini mwa Sahara zenye raslimali nyingi za misitu, lakini rais Lungu ameeleza wasiwasi kuwa kuendelea kwa ukataji miti bila udhibiti kunatishia mustakabali wa misitu ya nchi hiyo.

    Amesema mpango huo unalenga kuhimiza maendeleo ya uchumi kwa kutegemea miti ikiwa ni sehemu ya ajenda ya nchi hiyo ya kuepukana na kutegemea shaba peke yake, na kupunguza athari mbaya ya mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako