• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: AfDB kufanikisha ujenzi wa miundombinu Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-05-01 18:59:47

    Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) imeahidi kufanikisha ujenzi wa miundombinu muhimu na ya kisasa katika Jiji la Dodoma na mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler's Gorge.

    Ahadi hiyo ilitolewa na rais wa benki hiyo, Dk Akinumwi Adesina aliyekuwapo nchini kwa ziara ya siku tatu akihudhuria sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na kuzindua miradi kadhaa inayofadhiliwa na AfDB.

    Kwa kutambua umuhimu wa ushirikiano wa benki hiyo na Tanzania uliodumu tangu mwaka 1971 na kuiwezesha benki hiyo kuwekeza zaidi ya Dola 3.6 bilioni (zaidi ya Sh8 trilioni), Dk Adesina aliihakikishia Tanzania kuendelea kunufaika na misaada na mikopo yenye masharti nafuu kufanikisha mipango yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako