• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baadhi ya wafanyakazi waendelea na kazi katika siku ya mapumziko ya wafanyakazi

    (GMT+08:00) 2018-05-01 21:05:26
    Tarehe mosi Mei ni siku ya kimataifa ya wafanyakazi. Katika siku hii ya mapumziko, baadhi ya wafanyakazi wanaendelea na kazi ambazo haziwezi kusimama.

    Bw. Huang Xianbo ni kiongozi mtafiti wa kampuni moja ibinafsi. Tangu ajiunge na kampuni hiyo zaidi ya miaka 20 iliyopita, ameongoza kikundi chake kupata mafanikio mengi katika utafiti, na kuhimiza maendeleo ya teknolojia za safari ya anga ya juu na utengenezaji wa ndege kubwa nchini China. Bw. Huang anasema,

    "Napenda kazi maabara, kwani naweza kujifunza mambo mengi. Pia natarajia vijana wetu hodari wajiendeleze kwa haraka, kupata mafanikio zaidi katika uvumbuzi. Hivyo kampuni yetu itapata maendeleo endelevu."

    Katika siku ya kimataifa ya wafanyakazi, watu wengi wameenda kutalii katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Watibet kusini magharibi mwa China. Mjini Lahsa, polisi wa usalama barabarabi Bw. Pakhu yuko kazini. Anasema,

    "Kila mwaka wakati kama huu nakuwa nafanya kazi barabarani. Kuhakikisha utaratibu wa barabara ni jukumu langu. Ingawa nachoka baada ya kazi ya siku nzima, lakini nafurahia kazi yangu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako